July 15, 2022 SAMALEN TV
SHARE
Kupitia kongamano lao la wasanifu na watengenezaji wa programu lililofanyika siku chache zilizopita, kampuni ya Apple ilitangaza ujio wa mfumo mpya wa simu zao za iPhone baadaye mwaka huu. Mfumo huo, iOS 16 unalenga kufanya mabadiliko kutoka katika mfumo wao wa iOS 15 kwa kufanya maboresho ya baadhi ya huduma zilizopo katika mfumo huo pamoja na kuleta huduma mpya katika simu za iPhone.
Mfumo huu utaweza kupatikana katika matoleo yao ya kuanzia iPhone 8 na kuendelea. Hii inmaanisha matoleo yote kuanzia iPhone 7 kushuka chini hayatapata mfumo huo.
Kwa sasa, kampuni hio inaaanza kutoa toleo la majaribio la mfumo huo (IOS 16 Beta) ili kuangalia ufanyaji kazi wake na mfumo huo unategemewa kuzinduliwa rasmi kuanzia kwenye toleo lijalo la simu zao (iPhone 14 Series) mnamo mwezi wa tisa.
Muonekano wa Lock Screen.
Lock screen ni mpangilio wa picha na taarifa unaoonekana katika simu kaba ya kuifungua kwa PIN, alama za vidole, utambuzi wa uso ama namna yoyote ya Ulinzi iliyowekwa. Katika mfumo wa iOS16, eneo hili limepewa kipaumbele kikubwa, maana ni sehemu kubwa ambayo watumiaji wa simu hutazama katika matumizi ya simu zao.
Kwa kulitambua hili, kampuni ya Apple wameamua kuunda muonekano wa lock screen kitofauti kabisa ili kuwaaruhusu watumiaji kuweka mipangilio binafsi wanayoitaka, tofauti na ilivyozoeleka ambapo haikuwezekana kubadiisha chochoche zaidi ya picha. Mabadiliko katika lock screen ni haya yafuatayo.
Muonekano wa Saa katika lockscreen sasa waweza kubadilishwa ili kuendana na upendeleo binafsi
Rangi kuu katika picha iliyowekwa kwenye lock screen itaweza kutumika kama rangi ya maandishi yanayotokea katika lockscreen, hasa maandishi makubwa kama saa na tarehe
Sasa, utaweza kuweka ishara za taarifa muhimu (Widgets) katika lockscreen ili uweze kuzipata kwa urahisi.
Sasa, taarifa juu ya jumbe na vitu mbalimbali zinazoingia katika simu (Notifications) zitaonekana kutokea upande wa chini wa simu badala ya upande wa juu, baada ya saa kama ilivyozoeleka hapo awali.
Mabadiliko katika lock screen sasa yatafanyika kwa urahisi katika lockscreen yenyewe kwa kuigusa kwa sekunde chache tu ili kuonesha machaguo ya mabadiliko yaliyopo.
Kama picha uliyoweka katika lock screen ina mfumo wa Portrait, utaweza kusogeza mtu au kitu kilichowekewa umakini (focus) katika nafasi utakayoitaka.
Utaweza kutengeneza aina mbalimbali za lockscreen kutegemeana na miundo ya matumizi uliyoweka iwe kazini, au nyumbani na kuzifanya zitokee unapoweka muundo huo kutumika. BONYEZA HAPA KUJIUNGA NASI