MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI WA KUFANYA FIELD(MAZOEZI YA VITENDO) UKIWA CHUO 2023 - SAMALEN TV

SAMALEN TV

Trending on SAMALEN TV App

Notification texts go here Contact Us Buy Now!

MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI WA KUFANYA FIELD(MAZOEZI YA VITENDO) UKIWA CHUO 2023

Please wait 0 seconds...
Scroll Down and click on Go to Link for destination
Congrats! Link is Generated
Copyrighted by SAMALEN TV ©


Habari karibu kwenye article ya Leo naamini unayesoma ni kijana na mwanafunzi au mtu yoyote unayetegemea au uliyewahi kufanya field au mafunzo kabla ya kazi naitwa Samuel Efrem karibu Sana kwenye blog yetu Hakikisha unaacha comment yako hapa,maudhui haya yanapatikana kwenye app zetu zipakue sasa Kwa urahisi na kutumia gharama nafuu zaidi za bando bonyeza hapa APP YA TEKNOLOJIA 5G Hakuna wakati mzuri ambao unaweza kujifunza mambo mengi kama wakati wa mazoezi ya vitendo. Bahati mbaya wanafunzi wengi hawajui thamani ya muda huu. Wengi huona kama wanapoteza muda na hufanya mambo ili mradi tu siku ziende amalize muda wake wa mazoezi kwa vitendo. Faida kubwa ya muda wa mazoezi ya vitendo ni kwamba muda huo huwa unajifunza mambo ambayo utakuwa ukiyafanyia kazi ukiwa kazini. Mambo mengi unayojifunza darasani hautayatumia ukiwa kazini kikubwa utakachotumia ni kile unachojifunza katika mazoezi ya vitendo.

Mambo unayotakiwa kuyafanya muda wa mazoezi ya vitendo:
·        

  •  Wahi mapema katika eneo lako la kazi.

Tabia ya kuwahi kazini hautaijenga pale utakapo kuwa umeanza kazi bali unaijenga kabla ya kuanza kazi. Jitahidi kuamka mapema na kuwahi kila siku katika eneo lako unakofanyia mazoezi ya vitendo.


  • Waheshimu Watu wote.

Heshima haiuzwi dukani. Jitahidi kuwa na heshima katika eneo unalofanyia kazi, wasalimu watu wote bila kubagua vitengo vyao vya kazi. Siku moja wakati niko katika mazoezi ya vitendo dada mmoja aliniita na kuniambia maneno haya, “Wewe dogo mimi nakukubali sana.” Nikamuuliza kwanini? Akasema, “Nitafute baadae nitakwambia kwanini maana sasa hivi nina kazi nafanya.” Muda wa mapumziko nilimtafuta na kumuuliza kwanini alisema vile muda ule. Akaniambia, “Yaani wewe una heshima sana, wenzako huwa hata hawatusalimii na sijui kwa sababu sisi ni vibarua. Inaonekana kwenu ulifunzwa adabu vyema na mama yako.” Maneno yale yaliniingia kichwani na toka siku hiyo kila mtu ambaye huwa nikipishana naye nikiwa katika mazoezi ya vitendo huwa siachi kumpa salamu. Napenda kuwa mtu wa watu. Kumbuka watu wanajali endapo wakijua na wewe unawajali. Kanuni ipo hivyo.


  • Jifunze kutoka kwa mtu yeyote mwenye ujuzi

Kama ukiona mtu ana kitu fulani anakijua aisee chukua muda wako na jifunze kutoka kwake, haijalishi unamzidi umri au elimu wewe muombe akufundishe. Binafsi nimejifunza mambo mengi kutoka kwa mafundi wa ujenzi wakati wa mafunzo ya vitendo zaidi ya ninanvyo jifunza kwa injinia anayenisimamia. Jifunze kutoka kwa mtu yeyote utapata kujifunza mambo mengi. Niliwahi kukutana na kijana anayeitwa Shabani ambaye elimu yake ilikuwa ya kidato cha nne lakini alikuwa akifanya kazi katika maabara ya udongo inayohusiana na vipomo vya barabara, kijana yule alikuwa akijua mambo mengi yanayohusiana na barabara zaidi yangu mimi kwani nilikuwa ndo nimemaliza mwaka wa kwanza chuo hivyo muda mwingi nilikuwa nikifanya  kazi naye na nilijifunza mambo mengi kutoka kwake.


  •    Jitoe na fanya kazi kwa bidii

Mahali unapofanyia mazoezi kwa vitendo inaweza kuwa njia moja ya kukupa ajira endapo utakuwa mtu wa kujitoa na kufanya kazi kwa bidii. Ukijituma na kujitoa kwa uwezo wako wa hali ya juu watu unaofanya kazi nao watakupenda na muda wote watapenda kufanya kazi na wewe. Hakuna anayependa mtu mvivu. Kujituma na kufanya kazi kwa bidii muda wa mazoezi ya vitendo kunaweza kukufungulia fursa mpya ambazo hata hukuzitarajia. Kuna watu wengi wameajiriwa katika kampuni na taasisi ambazo walifanyia mazoezi ya vitendo. Sifa iliyowafanya wawe hapo ni kujituma, nidhamu na bidii waliyoionesha huko nyuma. Hata kama una ndoto ya kujiajiri kujituma ni suala la muhimu sana. Fanya kazi kana kwamba unaifanyia kampuni yako ili siku ujiajiri mambo uwe umekwisha yazoea kwamba kazi huwa zinafanywaje.


  •  Epuka Utoro

Kama umepangiwa kwenda kufanya mazoezi ya vitendo kila siku kwa wiki nane mfululizo epuka kuwa mtoro. Heshimu muda huo kana kwamba ni kazi yako ambayo tayari umekwisha ajiriwa na unapewa mshahara. Heshimu muda huo kana kwamba ni kampuni yako ambayo unaifanyia kazi na unahitaji kuingiza kipato. Ukifanya kazi kwa mtazamo huo hautakuwa na akili za kuwa mtoro. Utoro utakuchafua. Endapo utahisi kama hautaweza kufika katika eneo lako siku hiyo kwa sababu zilizo nje ya uwezo wako kama msiba au ugonjwa ni vyema ukatoa taarifa.


  •  Maliza kazi unazopewa mapema

Jitahidi kila unapopewa kazi uimalize mapema hii itakuongezea sifa kwa watu unaowafanyia kazi na pia itakuongezea uzalishaji. Jitahidi kuifanya kwa ubora pia usiwe mtu wa kukurupuka. Ukimaliza kazi uliyopewa omba kazi nyingine.


  • Ongeza muda wa ziada

Sio lazima kama umepangiwa na chuo chako kufanya mazoezi kwa vitendo kwa wiki nane ufanye kwa wiki nane basi. Kama una muda wa ziada unaweza kuongeza muda kama wiki moja au mbili. Hii inaitwa kujitolea na nimeizungumzia mara nyingi huko nyuma. Kujitolea ni alama za ziada unazojipatia na pia kunakuongezea sifa zaidi. Wanafunzi wengi wakikaguliwa huwa wanaacha kwenda kwenye maeneo yao ya mazoezi ya vitendo na hufikiri labda wanakikomoa chuo au msimamizi wao kumbe wanajikomoa wenyewe. Kama unautafuta utaalamu ni bora ukaongeza muda wa ziada. Kama unakumbuka vizuri kanuni ya masaa 10000, kuongeza muda ni chaguo bora sana kwako.


  • Usikate mawasiliano

Ukiwa katika eneo lako la mazoezi kwa vitendo ni wazi kwamba utakuwa umejenga urafiki na kufahamiana na watu mbalimbali. Ukimaliza muda wako endelee kuwasiliana na watu huo, urafiki wenu usiishie hapo. Huu ndio muda wa kuanza kujuana na watu mbalimbali. Hawa wanaweza kukufungulia milango ya fursa mpya.

"by Samuel Efrem(SAMALEN)

Niulize swali lolote kupitia comments nitakujibu!
This contains some of internet materials.

Getting Info...

Post a Comment

Your message is directed to SAMALEN TV
Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.